Russia imelaani mashambulizi yanayoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la kitakfiri la Daesh nchini Syria na kusema kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Alexander Lukashevich Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, Moscow inasisitiza kuwa hatua kama hizo zinaweza tu kuchukuliwa chini ya fremu ya sheria ya kimataifa ambapo kabla ya kuchukuliwa hatua hiyo ingepatikana ridhaa ya serikali ya Syria au kupasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa ripoti, Marekani na washirika wake wamefanya mashambulio karibu 200 ya anga dhidi ya wapiganaji wa Daesh nchini Syria. Mashambulizi hayo yamefanywa bila kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa, ingawa serikali ya Damascus imesema kuwa Marekani iliitaarifu
0 toamaon yako: