Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Rais wa CAR akutana na viongozi wa Anti Balaka

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Rais wa CAR akutana na viongozi wa Anti BalakaRais wa Serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti Balaka la nchini humo.
Taarifa kutoka Bangui zinasema kuwa, Rais Catherine Samba – Panza jana alikutana na viongozi wa kundi la Anti Balaka na kulitaka kundi hilo kuacha mara moja kukariri madai yao ya kumtaka ajiuzulu. Rais Samba – Panza ameongeza kuwa katika siku chache zijazo wananchi wa nchi hiyo watashuhudia amani na utulivu ikirejeshwa nchini humo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, siku chache zilizopita, mji mkuu wa nchi hiyo Bangui ulishuhudia mapigano yaliyosababisha watu wawili kuuawa raia wa Burundi na Cameroon na kusababisha askari sita wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kujeruhiwa kwenye mapigano hayo.
Wiki iliyopita, Patrice Edouard Ngaissona Mratibu wa kitaifa wa kundi la Kikristo la Anti Balaka alimtaka Rais Samba - Panza ajiuzulu kwa madai kwamba ameshindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yake.

         

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com