Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Mahamat Kamoun: Utulivu umerejea nchini CAR

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Mahamat Kamoun: Utulivu umerejea nchini CAR
Mahamat Kamoun, Waziri Mkuu wa muda wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza kuwa, amani na utulivu wa kiwango fulani umerejea katika nchi hiyo. Kamoun ametangaza kuwa, wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi kuanzia leo wanapaswa kurejea makazini na kuendelea na shugh uli zao kama kawaida. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, amri hiyo ya kuendelea na shughuli kama kawaida inazihusisha pia benki, maduka, mashirika na idara mbalimbali.
Wakati Waziri Mkuu huyo akitoa hakikisho la kurejea amani na utulivu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, taarifa kutoka nchini humo zinaonesha kwamba, hali ya usalama imeendelea kuzorota nchini humo. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, wakazi wa mji mkuu Bangui wameendelea kuukimbia mji huo. Siku ya Jumamosi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bangui ulifungwa kutokana na mapigano na machafuko yanayoendelea katika maeneo ya kaskazini mwa mji huo. Tangu mwaka 2012 Jamhuri ya Afrika ya Kati imetumbukia kwenye machafuko na mapigano ya kikabila ambapo Waislamu wamekuwa ndio wahanga wakuu wa machafuko hayo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com