Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 13

Jumatatu, Oktoba 13, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jumatatu, Oktoba 13, 2014Leo ni Jumatatu tarehe 18 Mfunguo 3 Dhilhija mwaka 1435 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 13 Oktoba mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1425 iliyopita yaani tarehe 18 Mfunguo Tatu, Mtume Muhammad (SAW) alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib (AS) kuwa Khalifa na kiongozi wa Waislamu baada yake. Siku hiyo Bwana Mtume alikuwa akirejea kutoka Makka alikokwenda kutekeleza ibada tukufu ya hija na iliyokuwa hija yake ya mwisho. Mtume alisimama mahala palipoitwa Ghadir Khum na baada ya kupanda sehemu yenye mwinuko aliuhutubia umma mkubwa wa Waislamu waliokuwa wamejumuika mahala hapo. Aidha Mtume (SAW) aliinua mkono wa Imam Ali na kusema: "Yule ambaye mimi ninayatawala mambo yake, huyu Ali ni Mwenye kuyatawala mambo yake pia, Ewe Mola! Mfanye kipenzi Mwenye kumfanya Ali kipenzi, mfanye adui Mwenye kumfanyia uadui na mnusuru mwenye kumnusuru." Ni kutokana na tukio hilo kubwa katika historia ya Uislamu, ndipo siku hii ikajulikana kuwa sikukuu ya Eidul Ghadir.
Siku kama ya leo miaka 2553 iliyopita mji wa kihistoria wa Babel ulitekwa na Korush, mwasisi wa utawala wa kizazi cha Hakhamaneshi nchini Iran. Ili kuweza kuudhibiti mji huo ambao ulikuwa na ngome kubwa na imara, Korush alitoa amri ya kubadilishwa njia ya maji ya Mto Tigris ambao ulikuwa ukipita ndani ya mji huo na kwa utaratibu huo askari wake wakatumia njia ya maji ya mto huo kuingia na kisha kuuteka mji huo. Mji huo ulioko kusini mwa eneo la Mesopotamia katika Iraq ya sasa ulikuwa katika kilele cha maendeleo na nguvu kubwa katika kipindi hicho.
Na miaka 50 iliyopita bunge la kimaonyesho la Iran lilipasisha sheria iliyowapa washauri wa kijeshi wa Marekani nchini kinga ya kutofikishwa mahakamani iwapo wangepatikana na hatia ya aina yoyote. Kwa mujibu wa sheria hiyo wahalifu wa Kimarekani wangehukumiwa nchini kwao kama watatenda jinai nchini Iran, na mahakama za Iran hazikuwa na haki ya kushughulikia kesi zao.
Sheria hiyo ilitambuliwa kuwa dharau kwa taifa la Iran na iliyokiuka wazi kujitawala kwa nchi. Kwa msingi huo hayati Imam Khomeini (MA) siku kadhaa baada ya kupasishwa sheria hiyo bungeni alitoa hotuba ya kihistoria akieleza taathira zake na kumshambulia vikali Mfalme Shah na Marekani. Baada ya hotuba hiyo Imam Khomeini alikamatwa na kupelekwa uhamishoni

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com