Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, September 29

Jumatatu, 29 Septemba 2014 Ghani aapishwa rais mpya Afghanistan

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Ashraf Ghani ameapishwa kuwa rais mpya wa Afghanistan, akichukua nafasi ya Hamid Karzai katika sherehe zilizofanyika ikulu ya rais mjini Kabul.
Kuapishwa kwa Bwana Ghani kunakuja baada ya miezi sita, huku kukiwa na mvutano mkubwa kuhusu kulalamikia udanganyifu katika kupiga na kuhesabu kura.
Kwa mujibu wa mkataba uliosimamiwa na Marekani Bwana Ghani atashirikiana madaraka na mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais Bwana Abdullah Abdullah ambaye atakuwa afisa mtendaji mkuu.
Kundi la Taliban limeupuuza mkataba huo kwa kuuita "igizo la Marekani". Mlipuko karibu na uwanja wa ndege wa Kabul umeua watu wapatao saba.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Sediq Sediqi amesema mtu aliyajilipua alishambulia kituo cha usalama cha ukaguzi katika barabara ya uwanja wa ndege inayoenda ubalozi wa Marekani.
Askari wanne wa usalama wa Afghanistan na raia watatu wameuawa na watu kadhaa kujeruhiwa, amesema.

Mabadiliko ya Kikatiba

Bwana Ghani ameapa kutii katiba katika sherehe za kuapishwa zilizohudhuriwa na viongozi 100.
Amesema atafanya kazi ya mpango wa amani ya muda mrefu, ameahidi kupambana na rushwa na kusema kuwa mabadiliko ya katiba yanahitajika.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com