Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba 2014 Makubaliano ya Iran, 5+1 yamefikiwa kwa asilimia 95

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Makubaliano ya Iran, 5+1 yamefikiwa kwa asilimia 95
Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa, mazungumzo ya nyuklia kat i ya Iran na kundi la 5+1 takriban yameshafikia kwenye hatua ya makubaliano ya mwisho kwa asilimia 95, na kwamba hivi sasa yamesalia masuala mawili - matatu ambayo bado ni magumu na nyeti kati ya pande hizo mbili. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa, masuala hayo yanaweza kutatuliwa, iwapo litaangaliwa suala hilo kiutaalamu zaidi. Naye Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, mazungumzo yalikuwa jaddi na ya uwazi na kusisitiza kwamba pande mbili zimebakiwa na miezi miwili ya kutatua hitilafu zilizosalia. Dakta Zarif amesisitiza kuwa, masuala yaliyosalia siyo magumu sana, kwani yanaweza kutatuliwa iwapo litawekwa kando suala la utashi wa kisiasa. Duru ya saba ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 linalozijumuisha nchi za Uingereza, Ufaransa, Russia, China, Marekani na Ujerumani ilimalizika siku ya Ijumaa mjini New York, bila ya kutangazwa matokeo ya mazungumzo hayo. Vyombo visivyo rasmi vinaeleza kuwa, duru ijayo ya mazungumzo itafanyika mwezi ujao barani Ulaya na kwamba huenda makubaliano ya mwisho yakafikiwa tarehe 24 Novemba mwaka huu.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com