Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba 2014 20:10 Rafsanjani: Muungano dhidi ya Daesh umeshindwa

Posted by mkachu  |  Tagged as: ,

Rafsanjani: Muungano dhidi ya Daesh umeshindwaMkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muundano dhidi ya kundi la Daesh katika eneo la Mashariki ya Kati umeshindwa.
Ayatullah Hashemi Rafsanjani amesema hayo leo katika kongamano la kwanza la kitaifa lililobeba jina la Vyuo Vikuu na Suala la Kujihami Kutakatifu hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, mashambulizi ya anga ya muungano huo wa kimataifa dhidi ya maeneo ya Daesh hayawezi kulimaliza kundi hilo la kigaidi na ushahidi ni kwamba siku chache zilizopita kundi hilo lilishambulia eneo la Kobani la Syria katika mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.
Ayatullah Rafsanjani aidha ameashiria namna Wamarekani wanavyokiri kuwa kama Iran haitausaidia muungano huo wa kimataifa dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, muungano huo hautoweza kulimaliza kundi hilo na kusisitiza kwamba: Marekani na waitifaki wake wameiwekea vikwazo Iran na huo ni moja ya uadui wao dhidi ya taifa la Iran, hivyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiwezi kuwa pamoja na Marekani na inafanya mambo yake kwa uhuru.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com