Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba 2014 20:09 Imarati yayashambulia vikali makundi ya kitakfiri

Posted by mkachu  |  Tagged as: ,

Imarati yayashambulia vikali makundi ya kitakfiri
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ameyashambulia vikali makundi ya kigaidi na kitakfiri katika eneo la Mashariki ya Kati akisema kuwa makundi hayo yanaonyesha picha mbaya kwa dini tukufu ya Kiislamu. Sheikh Abdullah bin Zayed Aal Nahyan amesema hayo wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani na kuongeza kuwa, vitendo vya makundi hayo ya kigaidi kama vile kuua watu kiholela, kuua watu kwa umati, kuteka nyara watu, kuwanyanyasa na kuwakandamiza vibaya wanawake na watoto wadogo wasio na hatia ni jinai, na kwamba Imarati inalaani vikali jinai hizo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu vile vile amesema, uhalifu wa kutisha unaofanywa na makundi hayo unakinzana kikamilifu na mafundisho ya Uislamu na kwamba makundi hayo yanafanya kosa kubwa yanapobeba bendera ya dini ili kuhalilalisha jinai zao. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Imarati pia amesema, nchi yake inalaani mbinu za kudhulma zinazotumiwa na makundi hayo yaliyojipachika jina la Uislamu kwani jinai na uhalifu wa makundi hayo unapingana kikamilifu na misimamo ya wastani na kuishi na watu wengine kwa usalama na amani

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com