Leo ni Jumapili tarehe 24 Mfungo Tatu Dhulhijjah mwaka 1435 Hijria, inayosadifiana na tarehe 19 Oktoba 2014 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 38 iliyopita, Ali Hassan Salameh mmoja kati ya viongozi wa juu wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO aliuawa shahidi nchini Lebanon kupitia njama za vibaraka wa Shirika la Ujasusi la utawala haramu wa Israel MOSSAD. Salameh alikuwa afisa wa usalama wa PLO na aliuawa shahidi baada ya kuripuka bomu lililotegwa katika gari lake mjini Beirut. Jinai hiyo ya utawala haramu wa Kizayuni ndani ya Lebanon kwa mara nyingine iliweka wazi ugaidi na uvamizi wa Israel dhidi ya ardhi ya nchi nyingine.
Siku kama ya leo miaka 11 iliyopita, alifariki dunia Ali Ezzat Begovic, mwanasiasa na mwandishi wa Bosnia Herzegovina. Ali Begovic alizaliwa mwaka 1925 na kupata taaluma ya sheria katika Chuo Kikuu cha Sarajevo katikati mwa Bosnia. Alianza kupambana na utawala wa kikomunisti wa Yugoslavia ya zamani akiwa kijana mdogo na kufungwa jela mara kadhaa. Mwaka 1989 Ali Begovic aliasisi chama kipya cha siasa kwa jina la Democratic Action kilichokuwa na nafasi kubwa katika uhuru wa Bosnia mwaka 1991. Mwanasiasa huyo wa Kiislamu ambaye baada ya uhuru wa taifa hilo alichaguliwa kuwa rais, alikuwa na nafasi kubwa katika kuwatetea raia wa Bosnia, katika mashambulizi ya askari wa Serbia na dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.
Na siku kama ya leo miaka 70 iliyopita, vita kati ya vikosi vya Japan na jeshi la Marekani vilianza katika visiwa vya Ufilipino. Itakumbukwa kuwa, wakati wa kuanza Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Ufilipino ilishambuliwa na Japan na kwa muda mfupi ikawa imedhibitiwa na kukaliwa kwa mabavu. Hata hivyo baada ya kushindwa Ujerumani ya Kinazi katika Vita vya Pili vya Dunia, majeshi ya Marekani chini ya usimamizi wa Douglas MacArthur yaliishambulia Ufilipino na kuyatoa majeshi ya Japan katika ardhi ya nchi hiyo na kisha kuanzisha kambi za kijeshi nchini humo.
0 toamaon yako: