Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 20

Jumamosi, Oktoba 18, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jumamosi, Oktoba 18, 2014Leo ni Jumamosi tarehe 23 Mfunguo Tatu Dhil-Hija 1435 Hijria inayosadifiana na tarehe 18 Oktoba mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, yaani tarehe 26 Mehr 1359 Hijria Shamsia, Shahidi Muhammad Ali Rajai Waziri Mkuu wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alihudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutoa hotuba ndefu kuhusu taathira zilizosababishwa na vita vya kulazimishwa vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa zamani wa Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Shahidi Rajai pia alizungumzia masuala muhimu ya dunia, hususan kukaliwa kwa mabavu Palestina na utawala wa Kizayuni pamoja na njama za wakoloni duniani kote. Baada ya hotuba hiyo, wawakilishi wa serikali ya Marekani walitaka kukutana na kufanya mazungumzo na shahidi Rajai, lakini Waziri Mkuu wa Iran alikataa pendekezo hilo kutokana na siasa za kibeberu za Marekani na jinai ilizotenda katika pembe mbalimbali duniani.
Katika siku kama ya leo miaka 83 iliyopita, msomi aliyegundua umeme aliyejulikana kwa jina la Thomas Edison alifariki dunia. Edison alizaliwa mwaka 1847 huko Marekani. Thomas Edison hakuwa na taalumu yoyote kutoka chuo kikuu bali ni tafiti na majaribio yake mengi pekee ndiyo yaliyopandisha juu kiwango chake cha elimu na maarifa. Akiwa kijana, Edison aliasisi maabara moja ya masuala ya kemia na kufanya majaribio makubwa katika maabara hiyo. Bidii ya msomi huyo ilimuwezesha kuvumbua mambo mengi ambapo muhimu kati ya hayo ni hatua yake ya kuvumbua umeme, kutengeneza lampu na gramafoni au santuri.
Miaka 92 iliyopita katika siku kama ya leo, redio ya BBC iliasisiwa huko Uingereza. Redio ya BBC awali ilikuwa ya mtu binafasi, lakini ilipofika mwaka 1927, redio hiyo ikawa chini ya usimamizi wa serikali na hivyo kuwa katika kalibu ya redio za serikali ya Uingereza. Bajeti ya redio za BBC ambazo zinatangaza kwa lugha mbalimbali za dunia inadhaminiwa na serikali ya Uingereza. Pamoja na kuwa BBC inadai kwamba haipendelei upande wowote katika matangazo yake, lakini katika kipindi cha nusu karne ya hivi karibuni, chombo hicho cha kupasha habari kimegeuka na kuwa wenzo wa serikali ya Uingereza na hivyo kuiandalia London uwanja wa kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.
Na miaka 76 iliyopita katika siku kama ya leo kulingana na kalenda ya Hijria, Sheikh Abbas Qumi alimu na mpokezi mashuhuri wa Kiislamu alifariki dunia. Alizaliwa mwaka 1294 Hijria katika mji mtakatifu wa Qum Iran. Awali Sheikh Abbas Qumi alisoma mjini Qum na baadaye akiwa na lengo la kujiendeleza zaidi katika masomo ya dini alielekea katika Chuo Kikuu cha Kidini cha Najaf Iraq. Akiwa Najaf, Sheikh Abbas Qumi alinufaika na bahari ya elimu ya wanazuoni mahiri wa zama hizo. Baadaye alirejea nchini Iran na kujishughulisha na kazi ya kualifu vitabu. Kitabu mashuhuri na chenye thamani kubwa cha Sheikh Abbas Qumi ni kile cha dua cha Mafatihul Jinan ambacho kina mkusanyiko wa dua na ziara.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com