Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Ijumaa, Oktoba 10, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Ijumaa, Oktoba 10, 2014Leo ni Ijumaa tarehe 15 Mfunguo Tatu Dhilhaji 1435 Hijria sawa na tarehe 10 Oktoba 2014 Milaadia.
Siku kama ya leo miaka 1221 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, alizaliwa Imam Ali Naqi (AS) mashuhuri kwa lakabu ya al-Hadi, mmoja wa wajukuu wa Mtume Muhammad SAW, katika mji mtakatifu wa Madina. Baada ya kuuawa shahidi baba yake, yaani Imam Jawad AS, Imam Hadi alichukua jukumu zito la Uimamu na kuongoza Umma wa Kiislamu. Zama za Uimamu wake zilisadifiana na kipindi cha utawala wa ukoo wa Bani Abbas, na Mutawakkil ndiye aliyekuwa ameshika hatamu za uongozi wakati huo. Baada ya mtawala huyo kuhisi kuwa Imam Hadi (as) na wafuasi wake walikuwa hatari kwa utawala wake, aliamrisha Imam atolewe Madina na kuhamishiwa Samarra, Iraq ili amuweke chini ya uangalizi. Licha ya hayo yote, lakini Imam Naqi aliendelea kueneza mafunzo sahihi ya dini tukufu ya Kiislamu.
Miaka 283 iliyopita katika siku kama hii ya leo mnamo mwaka 1731, alizaliwa huko katika mji wa Nice, Henry Cavendish, mwanafalsafa na tabibu wa Kiingereza. Cavendish alikuwa mwalimu wa masomo ya fikizikia, kemia na udaktari. Henry Cavendish alikuwa mtu wa kwanza aliyethibitisha kuwa gesi ya hyadrogen ni nyepesi zaidi kuliko hewa ya kawaida. Cavendish aliaga dunia m waka 1810.
Na miaka 112 iliyopita katika siku kama ya leo, kilifanyika kikao cha kwanza cha Mahakama ya Kimataifa ya Upatanishi ya Hague huko Uholanzi. Mahakama ya Upatanishi ya Hague iliundwa mwaka 1899 kufuatia pendekezo la Tezar Nicolaus wa Pili, Mfalme wa Urusi ya zamani. Mahakama hiyo ni moja kati ya taasisi za kisheria za kimataifa na iko chini ya Umoja wa Mataifa. Mahakama hiyo ina majaji 15 ambao huchaguliwa na Baraza Kuu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bila ya kutilia maanani utaifa wao.
Miongoni mwa majukumu ya Mahakama ya Upatanishi ya Kimataifa ya Hague, Uholanzi ni kutatua hitilafu kati ya nchi mbalimbali na kuzuia vita kati ya nchi hizo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com