Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Ebola:Hofu kwa watoto Marekani

Posted by mkachu  |  Tagged as:

  • Saa 3 zilizopita

Liberia ndio moja ya nchi zilizoathirika vibaya sana kutokana na Ebola
Watoto watano katika jimbo la Texas nchini Marekani waliokutana na mwanamume anayeugua Ebola nchini humo, wanachunguzwa kwa karibu nyumbani kubaini ikiwa wana dalili zozote za ugonjwa huo.
Kwenye mkutano na wandishi wa habari katika hospitali ya Texas Health Presbyterian mjini Dallas, gavana wa jimbo hilo alisema kuwa wazazi wa watoto hao wana wasiwasi lakini aliwahakikishia kuwa hakuna tisho la maambukizi.
Zaidi ya watu 3,000 wamefariki kutokana na Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi
Maafisa wamesema kuwa watoto hao wanachunguzwa kwa karibu na nkwamba kuna wanawachunguza watu wengine 12 au zaidi ambao huenda walikaribiana na mwanamume anayeugua Ebola.
Mgonjwa huyo Thomas Duncan anaaminika kuambukizwa Ebola alipokuwa nchini Liberia.
Duncan ni mgonjwa wa kwanza wa Ebola kupatikana nchini Marekani
Raia huyo wa Liberia aliingia nchini Marekani wiki mbili zilizopita kuwatembelea jamaa wake, na ni mtu wa kwanza kugunduliwa na Ebola akiwa nchini Marekani.
Bwana Duncan yuko katika hali mbaya kwa mujibu wa wahudum,u wa afya wanamuhudumia.
Kwa sasa yuko katika hali mbaya katika hospitali ya Texas Health Presbyterian
Muuguzi alimuuliza bwana Duncan alipotembelea hospitali lini alianza kujihisi mgonjwa na ikiwaaliwahi kuwepo katika eneo lililoathirika na Ebola.
Alimwambia kuwa alikuwa ametembelea Liberia, lakini taarifa aliyokuwa anatoa hakuwa ameitoa kwa kikosi kizima kilichohusika na matibabu yake hospitalini.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com