Ijumaa, 26 Septemba 2014 12:52
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa karibu watoto elfu kumi wanatumikishwa kama wanajeshi nchini Sudan Kusini. Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Kusini, Fatuma Ibrahim amesema kuwa mwenendo wa kuwatumikisha watoto katika vita nchini humo umeongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka huu licha ya makundi hasimu kuahidi kwamba yatasitisha suala hilo.
Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pilay pia mwezi Mei mwaka huu alisema kuwa pande mbili zinazopigana nchini Sudan zinawatumikisha watoto elfu 9 kama wanajeshi vitani na kwamba watoto wanauawa katika mashambulizi ya pande hizo mbili. Vilevile UNICEF na nchi nyingi za Kiafrika zimetia saini mkataba wa kushirikiana kwa ajili ya kuzuia mwenendo wa kutumikisha watoto vitani.
Kifungu nambari 38 cha Makubaliano ya Haki za Watoto kinasisitiza kuwa ni marufuku kwa makundi ya kisiasa kutumikisha vitani watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.
Utumiaji mbaya wa watoto unafanyika katika sura tatu. Kwanza ni kutumikisha watoto kama wapiganaji vitani, kuwatumikisha katika kazi za ulinzi, ujasusi na utumwa na kuwatumikisha katika kazi za kipropaganda wakati wa vita. Kwa sasa watoto wadogo wanatumishwa kwa wingi kama wapiganaji katika baadhi ya nchi za Afrika kama Somalia, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda na Burundi. Nchini Burundi mamia ya watoto wanafanyishwa kazi za kijeshi katika makundi ya waasi. Vilevile inasemekana kuwa jeshi la nchi hiyo limewasajili watoto wadogo.
Jumuiya za kimataifa zinapiga vita suala la kuwatumikisha watoto wadogo vitani na zinasisitiza juu ya udharura wa kokemshwa kabisa suala hilo. Umoja umetoa taarifa nyingi ukilaani hatua za kuwatumikisha vitani vitani watoto wenye chini ya umri wa miaka 18.
Hata hivyo wataalamu wa mambo wanaamini kuwa misimamo hiyo ya Umoja wa Ulaya ni kwa ajili ya kuzihadaa fikra za walimwengu. Wataalamu hao wanasema kuwa viongozi wa nchi za Magharibi ndio wanaochochea vita na mapigano katika nchi nyingi za Kiafrika kwa ajili ya kuhalalisha kuwepo kwa majeshi ya nchi hizo barani humo ambako wanatumiwa kupora utajiri na maliasili ya Afrika. Kuwepo kwa machafuko na mapigano hayo pia hutayarisha uwanja wa kutumiwa vibaya watoto wadogo kama watumwa, walinzi na wapiganaji vitani.
0 toamaon yako: