Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, September 25

Mashinikizo ya nchi za Kiarabu ya kutaka Israel ijiunge na NPT

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Mashinikizo ya nchi za Kiarabu ya kutaka Israel ijiunge na NPT
Nchi za Kiarabu zimetahadharisha kuhusu hatari ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel na kutaka Jamii ya Kimataifa ilichunguze na kulijadili suala hilo. Nchi hizo zimetangaza kuwa zitawasilisha rasimu inayosisitiza juu ya “Ulazima wa kukaguliwa vinu vya nyuklia vya utawala wa Kizayuni wa Israel” katika kikao kinachoendelea hivi sasa cha Baraza Kuu la Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA. Rasimu hiyo imetilia mkazo Israel kusaini mkataba unaopiga marufuku uundaji na uenezaji silaha za nyuklia (NPT). Sadiq Maarifi, mwakilishi wa Kuwait katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na mkuu wa kundi la wawakilishi wa nchi za Kiarabu katika wakala huo ameripoti kuwa katika kikao cha 58 cha Baraza Kuu la IAEA nchi za Kiarabu zitawasilisha rasimu ya azimio kuhusiana na suala la nyuklia la Israel. Kikao cha Baraza Kuu la IAEA kilianza siku ya Jumatatu na kinatarajiwa kumalizika rasmi hapo kesho. Sadiq Maarefi ameeleza kwamba kuchunguzwa suala la nyuklia la Israel ni jambo lenye udharura na ulazima kwa sababu vichwa vya nyuklia vya utawala huo ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati. Hatari ya nyuklia ya utawala wa Kizayuni wa Israel haihusiani na uundaji na urundikaji vichwa vya nyuklia tu bali kubwa zaidi ni kwamba uchafuzi wa nyuklia unaotokana na shughuli za viwanda vya nyuklia vilivyochakaa vya utawala huo ambavyo miale ya minururisho yake ya nyuklia inasambaa hadi masafa ya mbali vimesababisha hatari na madhara makubwa kwa eneo hili. Utawala wa Kizayuni wa Israel ndio utawala pekee katika Mashariki ya Kati ambao umekataa katakata kusaini mkataba wa NPT na kutouruhusu Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki uvifanyie ukaguzi vinu vyake vya nyuklia. Kushtadi hatari na uchafuzi wa nyuklia unaofanywa na utawala wa Kizayuni umezidisha hofu na wasiwasi kieneo na kimataifa; ukweli ambao unathibitishwa na kutiliwa nguvu na malalamiko yanayoongezeka kila siku ya nchi za ulimwengu na wito wao wa kutaka kuchunguzwa athari angamizi za shughuli za nyuklia za kijeshi za utawala huo haramu. Kuepushwa ulimwengu na hatari ya utawala wa Kizayuni, ambao ni utawala habithi na usio na chembe ya utu ni moja ya vipaumbele vikuu kimataifa, huku jumuiya za kimataifa zikiwa na mas-ulia makubwa juu ya suala hilo; na hilo ni jambo ambalo fikra za waliowengi duniani zimelitilia mkazo mara kadha wa kadha. Ukiukaji wa mara kwa mara wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala haramu wa Israel pamoja na waungaji mkono wake hususan kuhusiana na shughuli za nyuklia umeiweka hatarini pakubwa amani ya kieneo na kimataifa, hali ambayo inahitajia hatua za dhati na za haraka za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Hata hivyo kutokana na uafriti na pingamizi zinazowekwa na nchi za Magharibi jumuiya za kimataifa hadi sasa zimeshindwa kuchukua uamuzi wowote kivitendo dhidi ya utawala wa Kizayuni. Katika hali kama hii inachotarajia Jamii ya Kimataifa ni kwaona viongozi wa IAEA wakisimama imara na kutoathiriwa na ushawishi wa madola ya Magharibi na badala yake kuchukua hatua za haraka za kuchunguza hatari za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel na kutoruhusu utawala huo haramu uzidi kuhatarisha amani na usalama wa dunia…

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com