Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba 2014 Wanamgambo 123 wa Taliban wauawa Afghanistan

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Wanamgambo 123 wa Taliban wauawa AfghanistanSerikali ya Afghanistan imetangaza kuwa, kwa akali wanamgambo 123 wa kundi la Taliban wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mapigano makali kati ya majeshi ya serikali ya Kabul na wanamgambo hao katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan imetan gaza kuwa, majeshi ya serikali ya Kabul yamefanya operesheni kabambe katika mikoa tisa ya nchi hiyo na kuleta hasara na maafa makubwa dhidi ya kundi hilo. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, makamanda kadhaa wa kundi la Taliban wakiwemo Mulla Sirajuddin, Mulla Mir, Seifuddin Kuchi, Mulla Muhammad na Abdul Wadood maarufu kwa jinai la Zarqawi ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa kundi hilo waliouawa kwenye operesheni hiyo  na hasa katika majimbo ya Kunduz na Helmand. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, katika operesheni iliyofanyika katika mkoa wa Faryab ulioko kaskazini mwa Afghanistan, majeshi ya serikali yamefanikiwa kuwauwa makamanda  10 wa  kundi la Taleban. Duru hiyo imeeleza kuwa, majeshi ya serikali yamefanikiwa pia kukamata ngawira, zikiwemo silaha, zana za kijeshi na makumi ya pikipiki kwenye operesheni hiyo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com