Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, 28 Septemba 2014 OIC: Viongozi wa Israel washtakiwe kwa kutenda jinai

Posted by mkachu  |  Tagged as:

OIC: Viongozi wa Israel washtakiwe kwa kutenda jinai
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito wa kushtakiwa viongozi wa kijeshi na kisiasa wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu. Iyad Amin al Madani Katibu Mkuu w a OIC ameikosoa Israel kwa kuwafanyia Wapalestina vitendo visivyo vya kibinadamu kwa miongo kadhaa sasa. Amesema kuwa, kuna kesi kubwa ya kuitaja Israel kuwa ni utawala wa ‘ubaguzi wa rangi’ ambao unapaswa kushughulikiwa kimataifa. Al Madani ameongeza kuwa, wamekuwa wakifanya majadiliano ya kuishauri serikali ya Palestina kujiunga na Mkataba unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kuwa mwanachama wa korti hiyo. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia amesema, OIC inaunga mkono mpango wa Palestina wa kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liainishe muda wa kuondoka Israel katika ardhi inazozikalia kwa mabavu za Palestina.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com