Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, December 4

Yemen na ukwepaji jukumu la kulinda maisha ya wanadiplomasia wa Iran

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Yemen na ukwepaji jukumu la kulinda maisha ya wanadiplomasia wa IranKatika kuendelea kujiri matukio yanayotokana na kutojali serikali ya Yemen kulinda maisha ya wanadiplomasia na majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, makazi ya balozi wa Iran katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a jana yalilengwa na shambulio la kigaidi. Kwa mujibu wa duru za Yemen watu wasiopungua watatu akiwemo mlinzi wa nyumba ya balozi ambaye ni raia wa Yemen waliuawa na wengine kumi na saba walijeruhiwa, baadhi yao wakiwa mahututi kutokana na mripuko wa gari lililotegwa bomu ndani yake ambalo lilikuwa limeegeshwa karibu na nyumba ya Sayyid Hassan Niknam, balozi wa Iran mjini Sana'a. Balozi wa Iran hakuwepo nyumbani kwake wakati wa shambulio hilo ambalo lilisababisha pia hasara kubwa kwa nyumba za jirani na magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na mahali ulipotokea mripuko huo wa bomu. Kufuatia tukio hilo balozi mdogo wa Yemen hapa nchini alitakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Nje hapa mjini Tehran. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi za Kiarabu na za Kiafrika, Hussein Amir Abdolahian ameashiria kuitwa balozi huyo mdogo wa Yemen na kueleza kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imetoa indhari na sisitizo kubwa kuhusu jukumu la serikali ya Yemen la kulinda usalama wa wanadiplomasia na majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyoko mjini San’aa. Abdolahian ameongeza kuwa balozi mdogo wa Yemen amesisitiziwa kwamba matarajio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuona serikali ya Sana’a inachukua hatua za haraka za kumtambua, kumkamata na kumwadhibu mhusika au wahusika wa shambulio hilo la kigaidi. Shambulio la kigaidi la jana mbele ya makazi ya balozi wa Iran nchini Yemen limetokea katika hali ambayo kabla ya hapo wanadiplomasia wa Iran walishaandamwa na mashambulio kadhaa ya kigaidi ambapo katika kipindi cha karibu mwaka mmoja na nusu uliopita Nour Ahmad Nikbakht, Mwambata wa masuala ya uendeshaji wa ubalozi wa Iran nchini Yemen alitekwa nyara. Na kabla ya tukio la jana, mwanzoni mwa mwaka huu, Ali Asghar Asadi, mwanadiplomasia mwengine wa Iran aliuliwa wakati alipokuwa akikabiliana na magaidi waliokuwa wamedhamiria kumteka nyara. Licha ya ufatiliaji uliofanywa na maafisa wa Iran katika miezi ya hivi karibuni wa kutaka kujua hatima ya Nour Ahmad Nikbakht, Mwambata wa masuala ya uendeshaji wa ubalozi wa Iran mjini San’aa, hadi sasa viongozi wa Yemen hawajatoa jibu la kuridhisha juu ya suala hilo. Nayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilishawahi kumwita mara mbili balozi mdogo wa Yemen hapa nchini na kumweleza wasiwasi mkubwa ilionao Tehran juu ya hatima ya mwanadiplomasia wake huyo. Sambamba na hatua hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje Muhammad Javad Zarif alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen pembeni mwa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na akasisitiza tena juu ya jukumu ililonalo serikali ya Yemen la kuhakikisha mwanadiplomasia huyo wa Iran anaachiliwa huru haraka iwezekanavyo. Lakini mbali na wanadiplomasia wa Kiiran, wanadiplomasia wa nchi nyengine za kusini mashariki mwa Asia na wa nchi za Ulaya nao pia wamekuwa wakiandamwa na hujuma na mashambulio ya makundi ya kigaidi nchini Yemen. Hata hivyo badala ya viongozi wa serikali ya Yemen kufanya juhudi kwa ajili ya kuachiliwa huru mwanadiplomasia wa Iran aliyetekwa nyara na kuchukua hatua zinazotakiwa ili kulinda maisha ya wanadiplomasia, wamekuwa wakikwepa jukumu lao hilo na badala yake kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ati inaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo. Ukweli ni kwamba moja ya sababu kuu za kukosekana amani na usalama nchini Yemen ni udhaifu wa serikali ya muda ya nchi hiyo wa kushindwa kudhamini usalama na kuzuia uingizwaji silaha na makundi yanayobeba silaha nchini humo. Katika hali kama hiyo badala ya serikali ya Yemen kufanya juhudi zaidi za kulinda usalama wa raia wake na wa raia wa kigeni walioko nchini humo inajaribu kukwepa jukumu lake hilo na kuyahusisha matatizo yake ya ndani na nje ya mipaka ya nchi hiyo…

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com