Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Jumapili, Septemba, 28, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as: ,

Jumapili, Septemba, 28, 2014Leo ni Jumapili tarehe tatu Dhul-Hijja mwaka 1435 Hijria, inayosadifiana na tarehe 28 Septemba 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1073 iliyopita alizaliwa huko katika mji wa Birun karibu na Khorazm, moja kati ya miji ya zamani ya Iran Abu Raihan Biruni msomi, mnajimu na mwanahisabati mkubwa wa Kiirani. Abu Raihan Biruni alikuwa mtaalamu katika elimu za historia, jiografia unajimu na hisabati. Akiwa safarini nchini India, msomi huyo wa Kiirani alikutana na kufanya mazungumzo na maulamaa na watawala wa za ma hizo na baada ya kujifunza lugha ya Sanskrit ambayo ni lugha ya kale ya Kihindi Abu Raihan alikusanya taarifa muhimu alizokuwa akizihitaji kwa ajili ya kuandika kitabu chake alichokiita 'Tahqiq Ma Lilhind'. Mbali na kitabu hicho msomi huyo alipata kuandika vitabu vingi katika nyanja tofauti zikiwemo za unajimu na mantiki.
Siku kama ya leo miaka 123 iliyopita alifariki dunia mwandishi mashuhuri wa Kimarekani Herman Melville. Melville alizaliwa mwaka 1819 na kuanza kujishughulisha na ubaharia. Katika moja ya safari zake, meli ya Melville ilizama na kusukumwa na maji hadi katika kisiwa kimoja ambako wakazi wake walikuwa wakila watu. Melville ameelezea kisa hicho na jinsi alivyowatoroka watu hao katika kitabu alichokipa jina la Typee. Kuchapishwa kitabu hicho, kuliongeza zaidi umashuhuri wake.

Siku kama ya leo miaka 44 iliyopita, alifariki dunia rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser. Abdel Nasser alizaliwa mwaka 1916 Miladia. Aidha alishiriki katika vita vya kwanza vya Waarabu na utawala wa Kizayuni hapo mwaka 1948 na kufanya mapinduzi ya kijeshi kwa kushirikiana na Jenerali Najib, dhidi ya Mfalme Faruq 1952 na kuung'oa utawala wa kisultani nchini humo. Miaka miwili baadaye Gamal Abdel Nasser alimuondoa madarakani mshirika wake Jenerali Najib na kuchukua jukumu la kuiongoza Misri sanjari na kufanya juhudi za marekebisho, kupambana na ukoloni na utawala ghasibu wa Israel. Mwaka 1956 aliutaifisha mfereji wa Suez na kuufanya kuwa mali ya Misri, hatua iliyozifanya nchi za Ufaransa, Uingereza na utawala wa Kizayuni kuishambulia Misri. Hatua ya viongozi wa Misri ya kujibu hujuma hiyo, iliongeza umaarufu wa Abdel Nasser nchini Misri na ulimwenguni kwa ujumla.
Siku kama ya leo miaka 18 iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa azimio likiutaka utawala wa Kizayuni kukomesha operesheni ya kuchimba mashimo chini ya msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Rasimu ya azimio hilo ililaani uchimbaji huo wa mashimo kinyume cha sheria chini ya eneo hilo takatifu. Hata hivyo upinzani wa Marekani ulipelekea kuondolewa kipengee hicho katika azimio hilo.
Uchimbaji huo wa mashimo chini ya Msikiti wa al Aqsa na utawala huo ghasibu, ulizusha machafuko ya umwagaji damu mkubwa hapo tarehe 23 Septemba 1996 kati ya askari wa Israel na Wapalestina ambapo askari hao waliua na kujeruhi mamia ya Wapalestina.

Na siku kama ya leo miaka 14 iliyopita Intifadha ya wananchi wa Palestina kwa mara nyingine tena ilipamba moto. Hatua ya Ariel Sharon kiongozi wa chama chenye misimamo mikali cha Likud na mhusika mkuu wa mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika kambi za Sabra na Shatila ya kuingia katika Msikiti wa al Aqswa na kuuvunjia heshima msikiti huo mtukufu, iliwatia hasira Wapalestina na kuwafanya waanzishe maandamano na mapambano makubwa dhidi ya utawala huo wa Israel.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com