Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, October 12

Ubelgiji yakemea ndoa za kulazimishwa

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Ubelgiji yakemea ndoa za kulazimishwa Taasisi isiyo ya kiserikali nchini Ubelgiji imelaani vikali mwendelezo wa vitendo vya kuwalazimisha wasichana kuolewa wakiwa na umri mdogo duniani.
Taasisi ya Belgium Plan imeeleza kuwa, katika kila dakika moja wasichana wadogo 27 hufungishwa ndoa kwa nguvu duniani. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, vitendo hivyo vinashuhudiwa zaidi katika mabara ya Afrika na Asia. Vitendo vya  kuwalazimisha wasichana kuolewa wakiwa bado wadogo licha ya kuwazuia mamilioni ya wasichana hao kupata elimu na malezi bora, huhatarisha maisha yao kwa kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo.
Taasisi ya Belgium Plan imesisitiza juu ya udharura wa wasichana hao kupewa elimu na huduma afya. Hivi karibuni, Mfuko wa Watoto Duniani (UNICEF) ulitoa ripoti ukitangaza kuwa, zaidi  ya wasichana milioni 700 duniani walilazimishwa kuolewa wakiwa na umri mdogo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, karibu theluthi moja  kati ya watoto hao milioni 700 waliolewa wakiwa na umri wa miaka 15 tu.
 

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com