Leo ni Jumatano tarehe 6 Dhulhija 1435 Hijria inayosadifiana na tarehe Mosi Oktoba 2014.
Tarehe 6 Dhilhaji mwaka 1407
Hijria yaani siku kama ya leo miaka 28 iliyopita mamia ya mahujaji wa
Kiirani na mahujaji kadhaa wa nchi nyinginezo wa Nyumba ya Mwenyezi
Mungu waliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa serikali ya Saudi
Arabia, walipokuwa wakitekeleza faradhi ya kujibari na kujiweka mbali
na washirikina. Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu hutekeleza ibada
hiyo kila mwaka wakati wa Hija, kutokana na mafunzo ya Kiislamu na
Qur'ani Tukufu, ambapo sambamba na kutoa wito wa umoja na mshikamano
baina ya Waislamu, hutoa tangazo la kujiweka mbali na maadui wa Uislamu
hasa Marekani na utawala ghasibu wa Israel. Kwa kutilia maanani umuhimu
wa suala hiyo mwasisi
wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam
Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) daima alikuwa akisisitiza katika
ujumbe wake kwa wahujaji juu ya kufanya shughuli hiyo ya kujitenga na
washirikina na mabeberu, na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei pia amekuwa akisisitiza sana juu ya
umuhimu wa kufanyika kwake na kwamba inawaamsha Waislamu na kudhihirisha
uwezo na nguvu zao.
Miaka 29 iliyopita sawa na
siku kama ya leo ya tarehe Mosi Oktoba mwaka 1985 ndege za kijeshi za
utawala haramu wa Israel ziliyashambulia makao ya Harakati ya Ukombozi
wa Palestina (PLO) huko Tunisia. Watu wapatao 70 waliuawa na wengine
wengi kujeruhiwa kufuatia mashambulio hayo. PLO ilikuwa imehamishia
makao yake Tunisia kutoka Lebanon baada ya mashambulio ya kijeshi ya
utawala haramu wa Israel nchini humo mwaka 1982. Hata hivyo uungaji
mkono wa Marekani kwa utawala huo ulilifanya Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa lishindwe kuchukua hatua zozote za maana dhidi ya Tel Aviv.
Na Siku kama ya leo miaka 54
iliyopita, nchi ya Nigeria ilipata uhuru. Wareno waliwasili Nigeria
katika karne ya 15 na mkoloni Mwingereza naye akawasili katika nchi hiyo
katika karne ya 16. Katika karne ya 17 ardhi ya Nigeria iligeuzwa na
kuwa moja kati ya vituo muhimu vya biashara ya utumwa. Mwishoni mwa
karne ya 19 vikosi vya jeshi la Uingereza viliidhibiti kikamilifu ardhi
ya Nigeria. Mwaka 1914 Uingereza iliziunganisha nchi mbili za Nigeria ya
Kaskazini na Kusini zilizokuwa chini ya udhibiti wake na kuunda koloni
moja la Nigeria. Miaka 40 baadaye nchi hiyo ilijitangazia utawala wa
ndani. Hatimaye baada ya kupitia misukosuko mingi, Nigeria ilipata uhuru
katika siku kama hii ya leo.
0 toamaon yako: