China yaonya mataifa ya kigeni kutoingilia maswala ya Hong Kong
Uchina imesema kuwa haitawavumilia wahaini kutoka nje ya nchi wanaounga mkono maandamano yasiyo halali nchini humo.
Kundi
lijulikanalo kama Occupy Central ndilo linalolengwa kwa sababu limekuwa
likiunga mkono juhudi za maandamano ya maelfu ya watu wanaounga mkono
kuimraishwa kwa Demokrasia nchini Uchina.Katika kile kinachoaminika kulenga maandamano yanayoendelea katika jimbo la Hong Kon, Uchina inaonya mataifa mengine yasijiingize kwa kila inachoamini na maswala ya ndani ya Uchina.
Uchina mara kwa mara hutoa onyo kwa mataifa mengine yasijiingize katika jimbo hilo lake linalotaka kuendesha mambo yake kivyake.

Baraza Kuu la Kitaifa la Uchina, ambalo ni kiungo muhimu katika Serikali, limesema kuwa lina imani kwamba Serikali ya Jimbo la Hong Kong, ina uwezo wa kukabiliana na maandamano hayo kibinafsi bila kuingiliwa na yeyote.
Kuna hofu kuu Hong Kong kuwa huenda Serikali Kuu ikatumia polisi wenye silaha kuzima maandamano hayo.
0 toamaon yako: