
Amebainisha kwamba adui anataka kukabiliana na Uislamu wa kisiasa kwa kuzusha mfarakano na hitilafu baina ya Waislamu na pia kuanzisha harakati za kigaidi kwa jina la kidini na jihadi. Rais Rouhani ameongeza kuwa, kuoneshwa vitendo vya kikatili na kishenzi katika mitandao ya kijamii kwa madai ya Uislamu, ni njama zenye lengo la kuudhalilisha Uislamu katika dunia iliyostaarabika ya leo.
Katika upande mwingine, Rais wa Iran amekosoa vikwazo visivyo vya kibinadamu na vilivyo dhidi ya haki za binadamu vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutaka viondolewe. Pia amesema Tehran inashikamana na ahadi zake zote kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 mwezi Novemba, kama njia ya kujenga uaminifu.
0 toamaon yako: