
Taarifa kutoka Mogadishu zinasema kuwa, Ahmad Omar maarufu kwa jina la 'Abu Ubaida' ndiye kiongozi mpya wa kundi la al Shabab baada ya kuuawa Ahmed Abdi Godane katika shambulio lililofanywa na ndege za kijeshi za Marekani kusini mwa nchi hiyo iliyoko Pembe ya Afrika hivi karibuni.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Somalia kutangaza zawadi ya fedha kwa atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutiwa mbaroni kiongozi wa al Shabab. AbdulRahman Mahmoud Mkuu wa Shirika la Upelelezi na Usalama wa Taifa nchini Somalia ameahidi kwamba, shirika hilo halitatoa siri ya mtu yeyote atakayejitokeza na kufichua maficho ya Ahmad Omar kiongozi mpya wa al Shabab. Mahmoud amesisitiza kwamba, zawadi hiyo itatolewa kwa mtu atakayefanikisha kutiwa mbaroni kiongozi wa al Shabab akiwa hai au amekufa.
0 toamaon yako: