Mlima Ontake
Takriban
wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka
kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia
ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha mlima Ontake.
Zaidi ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwa mlima huo wenye urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila ya kutoa onyo lolote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.
0 toamaon yako: